HUYU NDIYE MUHAMMADU BUHARI; Alionekana kama mtu asiye na hisia, mkali

By Christina Mwakangale , Nipashe
Published at 08:09 AM Jul 14 2025
Muhammadu Buhari
Picha: Mtandao
Muhammadu Buhari

RAIS wa zamani wa Nigeria Muhammadu Buhari (82), amefariki dunia akiwa katika kliniki ya London, huko Uingereza.

Amewahi kuwa mtawala wa kijeshi na aliyejiita mwanademokrasia aliyebadili dini.

Alirejea madarakani kupitia uchaguzi lakini alijitahidi kuwashawishi wanigeria kwamba angeweza kutekeleza mabadiliko aliyoahidi.

Kamwe hakuwa mwanasiasa wa asili, alionekana kama mtu asiye na hisia na mkali. 

Lakini alibaki na sifa ya uaminifu wa binafsi, jambo adimu kwa mwanasiasa nchini Nigeria.

Baada ya majaribio matatu kufeli, Buhari alipata ushindi wa kihistoria mwaka 2015 na kuwa mgombea wa kwanza wa upinzani nchini humo kushinda.

Mwaka 2019, alichaguliwa tena kwa muhula mwingine wa miaka minne.

Buhari mara zote amekuwa maarufu miongoni mwa maskini wa kaskazini (inayojulikana kama "talakawa" katika lugha ya Kihausa) lakini kwa kampeni ya 2015, alikuwa na faida ya kundi lililoungana la upinzani nyuma yake.

Buhari mara zote amekuwa maarufu miongoni mwa maskini wa kaskazini (inayojulikana kama "talakawa" katika lugha ya Kihausa) lakini kwa kampeni ya 2015, alikuwa na faida ya kundi lililoungana la upinzani nyuma yake.

Pia alikuwa Waziri wa Mafuta, mwaka 1976 chini ya Rais Olusegun Obasanjo katika kipindi chake cha kwanza kama mkuu wa nchi wa Nigeria.

UTOVU WA NIDHAMU NA UFISADI

Kufikia 1978, Buhari, wakati huo kanali, alikuwa amerejea kuwa kamanda wa kijeshi. 

Msimamo wake mkali mwaka 1983, wakati baadhi ya visiwa vya Nigeria vilipochukuliwa katika Ziwa Chad na wanajeshi wa Chad, bado unakumbukwa kaskazini-mashariki, baada ya kulizingira eneo hilo na kuwatimua wavamizi.

Mwishoni mwa 1983 kulitokea mapinduzi mengine, dhidi ya Rais mteule Shehu Shagari, na Buhari, ambaye wakati huo alikuwa meja jenerali, akawa mtawala wa kijeshi wa nchi hiyo.

Kwa maelezo yake mwenyewe, hakuwa mmoja wa wapanga njama lakini aliwekwa (na hatimaye kutupwa) na wale waliokuwa na mamlaka halisi.

Ripoti nyingine zinaonesha alikuwa na jukumu kubwa katika kumwondoa Shagari kuliko alivyokuwa tayari kukiri.

Buhari alitawala kwa muda wa miezi 20, kipindi ambacho kinakumbukwa kwa kampeni dhidi ya utovu wa nidhamu na ufisadi, pamoja na ukiukwaji wa haki za binadamu.

Takribani wanasiasa 500, maafisa na wafanyabiashara walifungwa jela kama sehemu ya kampeni dhidi ya ubadhirifu na ufisadi.

Wengine waliona huu kama ukandamizaji mzito wa utawala wa kijeshi. Wengine wanakumbuka kama jaribio la kusifiwa la kupambana na ufisadi ulioenea ambao ulikuwa unarudisha nyuma maendeleo ya Nigeria.

UAMINIFU

Buhari alidumisha sifa adimu ya uaminifu miongoni mwa wanasiasa wa Nigeria, wanajeshi na raia, hasa kwa sababu ya kampeni hii.

Kama sehemu ya "vita vyake dhidi ya utovu wa nidhamu", aliamuru Wanigeria kupanga foleni nadhifu kwenye vituo vya mabasi, chini ya macho makali ya askari wanaotumia mijeledi.

Watumishi wa umma waliochelewa kazini walidhalilishwa hadharani kwa kulazimishwa kurukaruka kichura.

Baadhi ya hatua zake zinaweza kuonekana kuwa za kificho tu. Lakini nyingine zilikuwa za ukandamizaji wa kweli, kama vile amri ya kuzuia uhuru wa vyombo vya habari, ambapo waandishi wa habari walifungwa.

Serikali ya Buhari pia ilimfungia gwiji mkubwa wa muziki wa Nigeria, Fela Kuti, mwiba kwa viongozi waliofuatana, kwa madai ya uwongo yanayohusiana na mauzo ya fedha nje ya nchi.

CHANZO: BBC