Wanachama na viongozi mbalimbali wa Chama cha ACT-Wazalendo wamekusanyika katika Ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam kwa ajili ya Mkutano Mkuu wa chama hicho.
Mkutano huo mkubwa unalenga kumpata mgombea wa urais atakayewakilisha chama hicho katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.
Tukio hilo ni sehemu ya hatua muhimu za chama hicho katika maandalizi ya uchaguzi, ambapo wanachama kutoka mikoa mbalimbali nchini wanashiriki kujadili na kuamua hatma ya uongozi wa juu wa taifa kupitia ACT-Wazalendo.
Mkutano huo pia unatarajiwa kuwa jukwaa la kujadili ajenda kuu za kisera, kupitisha maazimio ya chama na kuimarisha mshikamano miongoni mwa wanachama.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED