Tume Huru ya Uchaguzi INEC imekitaka chama Cha ACT Wazalenndo kesho kiwasilisha fomu za uteuzi wa Rais katika ofisi ya tume hiyo zilizopo katika jengo la Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Jijini Dar es Salaam.
Hatua ya INEC kukiita chama hicho kupeleka fomu ya uteuzi imekuja baada ya jana Luhaga Mpina kushinda kesi ilitokana na malalmiko ya kada wa chama hicho Monalisa Ndala ya kupinga uhalali wa Mpina kugombea Urais.
Taarifa iliyotolewa na tume hiyo kwa umma leo na kuitwa saini na Kaimu Mkurugenzi wa Uchaguzi, Juma Rahisi imekikumbusha chama hicho kuzingatia masharti ya kanuni 20(4) ya uchaguzi wa Rais, wabunge na madiwani za mwaka 2025 inayowataka wagombea kufika katika ofisi hizo wakiwa na:
Fomu zao za uteuzi zilizojazwa kikamilifu, picha nne za rangi zenye ukubwa sawa na picha inayotumika kwenye pasi ya kusafiria zenye mwonekano mweupe kwa nyuma, uthibitisho wa stakabadhi ya malipo ya dhamana ya kiasi cha Sh Milioni moja na fomu namba 10 ya tamko la kuheshimu na kutekeleza maadili ya uchaguzi ya Rais, wabunge na madiwani ya mwaka 2025 itakayojazwa na kusainiwa mbele ya Mkurugenzi wa Uchaguzi.
Aidha taarifa hiyo imekitaka chama hicho wakati wa kurudisha fomu kuzingatia mambo yafuatayo ikiwamo wagombea waliopendekezwa wasifike na watu zaidi ya kumi.Mengine ni wafike na magari yasiyozidi matatu, kutofanya maandamano na shamrashamra nje ya ofisi ya tume, hakutakuwa na fursa ya kuongea na waandishi wa habari, kutoa orodha ya watu wasiozidi kumi kwaajili ya lojistiki za mapokezi.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED