Balile, Machumu wachaguliwa kuendelea na nafasi zao

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 02:23 PM Apr 05 2025
Deodatus Balile (kushoto) na Bakari Machumu (kulia)
PICHA: MTANDAO
Deodatus Balile (kushoto) na Bakari Machumu (kulia)

Wanachama wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), wamewachagua Deodatus Balile na Bakari Machumu kuendelea na nafasi zao kwa miaka minne ijayo.

Balile ambaye amegombea nafasi ya Mwenyekiti na Machumu Makamu Mwenyekiti,walichaguliwa baada ya kujieleza mbele ya wanachama 147.

Kutoka na kwamba kwenye nafasi hizo hakukua na wagombea wengine,na kanuni za uchaguzi zinataka kuwepo pingamizi ndipo zipigwe kura za ndio na hapana.

Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi,Frank Sanga alitangaza kwa mujibu wa kanuni ya saba na nane hakukua na pingamizi, hivyo aliwatangaza Balile na Machumu kuwa washindi wa nafasi hizo kuongoza kwa miaka minne ijayo.

Aidha,TEF imeendelea kuchagua wajumbe wa Kamati ya Utendaji ambao wagombea ni 12 na kikatiba wanatakiwa wapatikane saba.