Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesema katika siku 100 za uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan akiingia madarakani kutaanzishwaTume ya Maridhiano ili Watanzania wawe kitu kimoja.
Mgombea Mwenza wa Urais wa CCM, Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi ameeleza hayo leo Septemba 03 eneo la Lalago mkoani Simiyu. Alipofanya mkutano ikiwa ni mwendelezo wa kampeni za Uchaguzi Mkuu.
Balozi Dk. Nchimbi amesema: "Katika mambo ambayo Serikali ya CCM itayafanya ndani ya siku 100 ni kuanzishwa kwa Tume ya Maridhiano ili Watanzania wote wasikilizwe, amani, umoja uendelezwe. Watanzania wote tuwe kitu kimoja. Wale wengi wasikilizwe, wale wachache wasilizwe. Tunataka nchi iwe na watu wanaosilizana, wanaoelewa na kusikilizana"
Pamoja na mambo mengine, Balozi Dk. Nchimbi amesema serikali pia itaanzisha mfumo wa mawasiliano nchini utakaorahisisha wananchi kuwasilisha kero zao kwa wakuu wa wilaya, mikoa.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED