Makamu Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo Zanzibar Ismail Jussa Ladhu amesema kuna haja ya kutazamwa upya mfumo wa Muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar ili uweze kuleta usawa kwa pande zote mbili licha ya kuwa watawala hawapo tayari kwa sababu ya maslahi yao.
Ismail Jussa ameyasema hayo wakati akihutubua maelfu ya vijana wa Chama hicho katika kongamano maalumu la kuadhimisha miaka 61 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar lililofanyika ukumbi wa Samail Gombani Chake chake Pemba.
"Nyinyi vijana wa Zanzibar wakati leo tunaadhimisha miaka 61 ya Muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar mna wajibu mkubwa wa kurudisha heshima yenu na Nchi yenu ya Zanzibar kutoka kwenye Muungano huu usiokua na usawa" Ismail Jussa.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED