WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa, amesema hali ya siasa na utekelezaji wa demokrasia nchini, imeendelea kuimarika kutokana na maboresho ya mifumo na jitihada mbalimbali za makusudi zinazofanywa na serikali.
Amesema moja ya jitihada hizo ni marekebisho ya sheria mbalimbali kwa lengo la kuimarisha utawala wa demokrasia hapa nchini.
Majaliwa amesema hayo leo, bungeni jijini Dodoma, wakati akisoma hotuba ya bajeti ofisi yake kwa mwaka wa fedha 2025/2026.
“Aidha, mweashimiwa Naibu Spika, Bunge lakoTukufu lilitunga Sheria ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Na. 1 ya Mwaka 2024, Sheria ya 68 Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani Na. 2 ya Mwaka 2024 na kufanya Marekebisho ya Sheria ya Vyama vya Siasa Sura ya 258.
“Serikali kwa upande wake tayari imeshakamilisha utungaji wa Kanuni za Sheria ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi.”
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED