Mwili wa mtu mmoja uonekana Jangwani, Dar

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 06:14 PM Aug 27 2025
Mwili wa mtu mmoja uonekana Jangwani, Dar

Mwili wa mtu mzima umeonekana mapema asubuhi ya leo Agosti 27,2025 ukiwa unaelea kwenye mtaro karibu na kilipokuwa kituo cha mabasi ya mwendokasi, huku eneo hilo likiwa na ujenzi wa barabara mbadala kabla ya kubomolewa kwa barabara ya awali kwa ajili ya daraja la juu litakalounganisha Fire na Magomeni.

Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Peter Mabusi, amesema walipokea taarifa saa 3:30 asubuhi na timu ya uokoaji ilitumwa kufuatilia. Walikuta mwili wa marehemu Swalehe Shukurani chini ya daraja lenye maji na kuutoa saa nne kasoro asubuhi, kisha kukabidhiwa Jeshi la Polisi kwa uchunguzi zaidi katika Hospitali ya Polisi Barabara ya Kilwa.

Mabusi amesema mwili umetambuliwa na majirani waliotokea eneo la tukio, huku Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro, akisema uchunguzi unaendelea na taarifa kamili zitatolewa baada ya kukamilika.