‘Naisikia sauti ya Mungu, siukimbilii urais kwa masilahi yangu’

By Elizabeth Zaya , Nipashe
Published at 02:47 PM Sep 07 2025
Mgombea Urais wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), Salum Mwalimu
Picha: Elizabeth Zaya
Mgombea Urais wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), Salum Mwalimu

SALUMU Mwalimu: "Siukimbilii urais kwa sababu nautamani kwa masilahi yangu, ila naisikia sauti ya Mungu, ikiniambia nenda kawasaidie watanzania wenzako na hiyo ndio inanipa ujasiri."

"Nchi hii imejaliwa kila aina ya neema, madini kila kona, bahari, mito na ardhi takatifu, nchi imejaliwa vivutio vya kila aina na rasilimali ya kila aina  ambayo unatamani nchi iwe nayo, lakini bado ni masikini.

"Tanzania ina utajiri wa rasilimali ambao baadhi ya mataifa haiufikii hata robo lakini ni tajiri, hii haikubaliki."

Mgomnbea urais kupitia Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), Mwalimu ametoa kauli hiyo, leo, Septemba 7, 2025 wakati akizungumza kwenye mkutano wa kampeni, mjini Babati mkoani Manyara na kuwaomba watanzania wamchague, ili akibadilishe Tanzania.