Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) umedhamini mbio Maalum kusherehekea kilele cha miaka 61 ya Muungano wa Tanzania, hapa mkoani Singida
Mbio hizo za kilomita 10 na killomita 5 ziliongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Singida Halima Dendego na kuhudhuriwa na Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Singida, Martha Mlata, Wakuu wa Wilaya, Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), Hery Mkunda, Wafanyakazi wanaoshiriki Maonesho kuelekea Kilele cha Mei Mosi na Wananchi.
Mbio hizo zilifanyika katika Viwanja vya Chuo cha VETA.
Akizungumza katika tukio hilo, RC Dendego alisema, "Ninawapongeza washiriki wote wa mbio hizi, tumepata bahati mbio hizi zinafanyika katika wiki ya kuelekea kilele cha sherehe za Mei Mosi ambazo kitaifa zitafanyika hapa mkoani Singida, lakini pia Mbio hizi zinaenzi miaka 61 ya Muungano wetu.”
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED