Rais Samia: Tumempoteza kiongozi mahiri, Mwanamajumui wa Afrika

By Christina Mwakangale , Nipashe
Published at 12:40 PM Oct 15 2025
Rais Samia Suluhu Hassan
Picha: Mtandao
Rais Samia Suluhu Hassan

Rais Samia Suluhu Hassan, ametoa salamu za rambirambia kufuatia kifo cha Raila Odinga, kilichotokea leo.

Kwenye ukurasa wake mtandaoni amesema: "Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha Raila Amolo Odinga.Tumempoteza kiongozi mahiri, Mwanamajumui wa Afrika, mpenda amani na mtafuta suluhu, ambaye ushawishi na upendo wake haukuwa tu ndani ya Kenya, bali Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla. 

"Msiba huu si wa Kenya pekee, bali wetu sote. Kwa niaba ya serikali na wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ninatuma salamu za pole kwa Rais wa Jamhuri ya Kenya, Dk. William Samoei Ruto, Mama Ida Odinga, watoto, familia, ndugu, jamaa, marafiki na wananchi wote wa Kenya kwa msiba huu.

"Tunaungana kuwaombea kwa Mwenyezi Mungu awajalie subra, faraja na imani katika kipindi hiki, na ailaze roho ya mpendwa wetu, Mheshimiwa Raila Amolo Odinga, mahali pema peponi. Amina."