Mgombea urais wa Chama cha Ukombozi wa Umma(CHAUMMA), Salum Mwalimu, amewaahidi Watanzania kwamba hatowaangusha endapo watamwamini kupitia sanduku la kura 29 mwezi aiongoze Tanzania.
Mwalimu ametoa kauli hiyo leo kwenye mkutano wa kampeni wa kusaka kura ikiwa ni wiki za lala salama kupeleka kwenye uchaguzi huo mkuu wa nchi wa kuchagua rais, wabunge na madiwani.
Amesema amejipanga na yuko vizuri kwenye suala la uchumi na atahakikisha anatengeneza uchumi wa kipato kwa wananchi wake.
"Na hilo ninawahakikishia, wanaweza kunishindaka mambo mengine lakini kwenye suala la uchumi hawanishindi, sitawangusha Watanzania, naomba waniamini Oktoba 29,"alisema Mwalimu.
Pia, Mwalimu amesema jambo jingine atakalolifanya ni kulinda utajiri asili wa eneo husika kwa kuhakikisha unawanufaisha wenyeji kwanza kabla ya kupelekwa sehemu nyingine.
"Mfano, kama watu wa Kilimanjaro au Kaskazini wanavyonufaika na Mlima Kilimanjaro kwanza, ndivyo itakavyokuwa kwenye uongozi wangu."
"Ndivyo itakavyokuwa kwenye itawapa wangu, mfano mikoa yenye gesi asili, ndio inatakiwa ianze kunufaka kabla ya kupelekwa sehemu nyingine au mikoa mwingine."
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED