Mgombea urais wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), Salum Mwalimu, amesema kuwa endapo atachaguliwa kuwa rais, atasitisha mipango yote ya kuhamisha gesi kutoka mikoa ya Kusini kwenda kuchakatwa nje ya mikoa hiyo.
Mwalimu amesema hayo leo, Oktoba 15, 2025, katika mkutano wa kampeni uliofanyika Lindi, akisisitiza kuwa gesi itachakatwa ndani ya mikoa hiyo ya Kusini, huku viwanda vya kuchakata gesi vikijengwa katika maeneo hayo ili kuunda ajira na kuongeza uchumi wa wenyeji.
“Nitataka gesi ichakatwe katika mikoa hiyo hiyo ya Kusini na tutajenga viwanda vya kuichakata huku, ili tutengeneze ajira na uchumi wa wenyeji wa eneo husika kabla ya kupelekwa eneo jingine,” amesema Mwalimu.
Amesema lengo la mpango huu ni kuhakikisha wananchi wa maeneo husika wanapata faida za kiuchumi kabla ya rasilimali hizo kusafirishwa nje.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED