Wenje: Ukisalimiwa jibu ‘Oktoba Tunatiki’

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 03:37 PM Oct 15 2025
Kada mpya wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ezekia Wenje.

Kada mpya wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ezekia Wenje ametaka kauli ya ‘Oktoba Tunatiki’ iwe jawabu la salamu ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha Watanzania kujitokeza Oktoba 29 kumpigia kura mgombea wa CCM,Samia Suluhu Hassan.