TPDC washuhudia zilipo hatua EACOP

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 03:09 PM Oct 12 2025
Viongozi wa Bodi ya Wakurugenzi wa TPDC, wakiongozwa na Mwenyeki wa bodi hiyo, Balozi Ombeni Sefue, wakikagua ujenzi wa mradi huo.
Picha Boniface Gideon
Viongozi wa Bodi ya Wakurugenzi wa TPDC, wakiongozwa na Mwenyeki wa bodi hiyo, Balozi Ombeni Sefue, wakikagua ujenzi wa mradi huo.

‎BODI ya Wakurugenzi Shirika la Petroli Tanzania (TPDC), imeridhishwa na kasi ya ujenzi na matengenezo ya mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi Afrika Mashariki (EACOP).

Mradi huo umefikia asilimia 72, huku ukitarajiwa kuanza rasmi kufanya kazi ifikapo Juni 2026.

‎Akizungumza na waandishi wa habari jana, jijini Tanga, mara baada ya bodi hiyo kumaliza ukaguzi katika wilaya zinazopitiwa na mradi huo katika mkoa wa Tanga.

‎Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TPDC, Balozi Ombeni Sefue, amesema mradi huo umeonesha ukomavu wa mataifa mawili ya Afrika Mashariki katika sekta ya uwekezaji,

‎"Mradi huu wa EACOP ndio mradi bora  zaidi wa mafuta kwasasa Duniani na umefuata taratibu zote za Kimataifa,mradi huu umeonyesha ukomavu na uimara wa mataifa ya Afrika Mashariki," amesisitiza Balozi Sefue.

‎Balozi Sefue amesema haikuwa kazi rahisi kupata mradi huo, kutokana na ushindani mkubwa uliokuwapo kwenye mataifa mbalimbali.

Mwakilishi wa Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya mafuta ghafi EACOP, Georfrey Mponda, amesema mradi huo ulianza rasmi utekelezwaji Februari 15, mwaka 2022 na unatarajiwa kukamilika jun 2026 nakwamba mpaka sasa mradi huo umefikia asilimia 72 ya ujenzi.