Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji wa Mahakama ya Rufani, Jacobs Mwambegele akizungumza wakati wa kikao cha pamoja kati ya Tume na Wadau wa Uchaguzi Halmashauri ya Wilaya ya Singida mkoani Singida kilicholenga kuthibitisha kuwa maombi yaliyowasilishwa ya mapendekezo ya kubadili jina la jimbo Singida Kaskazini, Halmashauri ya Wilaya ya Singida Mkoa wa Singida ni sahihi kwa mujibu wa barua iliyowasilishwa na Katibu Tawala wa Mkoa.
Jaji Mwambegele aliwaambia kuwa baada ya kufanyika kwa kikao hiko, haina maana kwamba ombi leo limekubaliwa, bali tume imetimiza matakwa ya kanuni ya 18 ya Kanuni za Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi za mwaka 2024 za kutembelea majimbo yaliyoomba kugawanywa au kubadili jina la jimbo.
“Hivyo, tume itakutana na kuendelea kuchakata taarifa zote na baada ya hapo kwa kuzingatia masharti ya Katiba na Sheria, itatangaza majimbo yaliyogawanywa na au kubadilisha majina,”alisema Jaji Mwambegele.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED