Ukimya wa serikali waishtua NETO

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 04:50 PM Apr 26 2025
Mwenyekiti wa umoja wa walimu wasiokuwa na ajira Tanzania kuanzia mwaka 2015 hadi 2023 (Neto) Joseph Kaheza
PICHA: MTANDAO
Mwenyekiti wa umoja wa walimu wasiokuwa na ajira Tanzania kuanzia mwaka 2015 hadi 2023 (Neto) Joseph Kaheza

Umoja wa Walimu Wasio na Ajira Tanzania (NETO), imesema licha ya kwamba siku 45 za ahadi ya serikali zimekamilika leo Aprili 26,2025,lakini hawajapokea mrejesho wowote hadi sasa.

Taarifa kwa umma iliyotolewa leo Aprili 26,2025 na Katibu Mkuu wa NETO, Daniel Mkinga, imesema kuwa kwasasa wanaomba maoni ya wanachama wao juu ya nini kifanyike baada ya ukimya wa serikali.

"Viongozi wa NETO kupitia kwenye magroup yetu tumendaq utaratibu wa kupokea maoni juu ya nini kifanyike kwa kuwa siku 45 zimekamilika na hatujapokea mrejeshi kutoka serikalini,"amesema na kuongeza:

"Tunawaomba sana mshiriki kikamilifu kutoa maoni yenu ambayo viongozi watayatumia katika kutetea haki zenu.Maoni yataanza kupokelewa leo Aprili 26,2025 baada ya viongozi kutoa utaratibu wa ukusanyaji maoni."

Aidha,Mkinga amesema viongozi wa NETO walo imara na wataendelra kusimamia malengo na dhumuni la uanzishwaji wa umoja huo,ikiwamo kudai haki ya ajira pasipo kuvunja sheria za nchi,kutumia njia zinazoweza kuharatqrisha au kuvuruga amani na utulivu wa nchi.