Mwenyekiti wa Muungano wa Vyama Vikuu vya ushirika wa wakulima wa korosho kanda ya kusini, Odas Mpunga amevitaka vyama vya msingi vya wakulima kuwa na mpango dhabiti ya uanzishaji wa miradi ya maendeleo na kuondokana na utegemezi wa ushuru.
Mpunga alisema hayo Wakati akiongea na wajumbe wa mkutano mkuu wa kawaida wa 22 uliofanyika katika ukumbi wa Sky way mjini hapa. Akifafanua taarifa hiyo Mpunga alisema kuwa Bila Amcos hizo kuwa na mopango endelevu iwezekakano wa KUPIGA hatua kwa kitegemea ushuru utakuea ni mgumu sana.
Alisema kwa kuanzia tayari Vyama Vikuu vyote vya MAMCU,RUNALI,,TAMCu na TANECU VILIVYOPO katika ukanda huo vimeanza kuonesha njia lea kununua malory pamoja na kujenga miradi ya viwanda na Hoteli kama sehemu ya mikakati ya kujiondoa kwenye utegemezi wa ushuru .
Pamoja na maelezo hayo Mpunga pia akatumia nafasi hiyo kuipongeza serikali ya awamu ya sita kwa kutoa viatiligi na pembejeo za ruzuku kwa kipindi cha miaka 3 mfululizo na kusaidia kuwapimguzia adha Wakula wa korosho.
Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi ccm wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma Abdalah Mtila alisema kuwa utekelezaji na usimamozi wa viongozi WA chama kikuu Cha ushirika wilaya ya Tunduru TAMCU katika usimamozi na igawaji wa pembejeo umesaidia kupunguza kero kwa wananchi ambao kwa sehemu kubwa ni wakulima wa zao hilo.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED