Wananchi Tunduru wagombea kadi za CHAUMMA kama 'njugu'

By Elizabeth Zaya , Nipashe
Published at 12:14 PM Jul 17 2025
Wananchi Tunduru wagombea kadi za CHAUMMA kama 'njugu'

Wananchi wa Tunduru, mkoani Ruvuma leo wamejikuta wakigombania kadi za kuomba uanachama wa Chama cha Ukombozi wa Umma(CHAUMMA).

Tukio hilo limetokea leo baada ya viongozi wa chama hicho kuzungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika mjini Tunduru.

Baada ya kumaliza kuzungumza, viongozi wa chama hicho walijikuta katika wakati mgumu baada ya idadi kubwa ya wananchi kuwakimbilia ili wapewe kadi za uanachama huku wengine wakivamia jukwaa.

Kutokana na hali hiyo iliwabidi viongozi wa chama hicho kuanza kuwaomba watulie na wasubiri kuwekewa utaratibu mzuri ili kila mtu apatiwe kadi  ambapo  wengine walifikia hatua ya kunyang'anyana kadi na kila aliyeipata alikwenda kupanga foleni kwa ajili ya kuandikisha jina kwa ajili ya kuomba kujiunga na chama hicho.