JK, Mwinyi waupa kongole mchakato upatikanaji Dira yaTaifa 2050

By Renatha Msungu , Nipashe
Published at 04:14 PM Jul 17 2025
Rais Mstaafu Jakaya Kikwete (kushoto) na Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Wawakilishi, Dk. Hussein Mwinyi
Picha: Nipashe Digital
Rais Mstaafu Jakaya Kikwete (kushoto) na Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Wawakilishi, Dk. Hussein Mwinyi

RAIS Mstaafu Jakaya Kikwete, amesema,mchakato wa uandaaji wa Dira ya Taifa 2050, umefanyika kwa weledi na ukiwa shirikishi.

Kikwete amesema dira hiyo, inaakisi mahitaji, matarajio na matumaini ya nchi, hivyo NI Dira ambayo itaitoa Tanzania katika uchumi wa kati kwenda uchumi wa juu.

Amesema hayo katika uzinduzi wa Dira ya Taifa 2050 iliyofanyika leo, Julai 17, 2025, jijini Dodoma 

"Naipongeza sana serikali pamoja na timu iliyohusika kuandaa Dira ya Taifa ya 2050, naamini inamgusa kila mmoja," amesema Kikwete.

Naye Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Wawakilishi, Dk. Hussein Mwinyi, ametoa  wito kwa watanzania kupokea dira hiyo, kwa matumaini, kwa kuwa inagusa maisha ya watanzania katika masuala mbalimbali.

Amesema imezingatia kuleta maendeleo kwa kila mtanzania na taifa kwa ujumla, hivyo ni wajibu wa kila mmoja kuelewa  wajibu wake katika kufanikisha utekelezaji mahiri wa dira hiyo.