Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Stephen Wasira amemjibu mwanasheria wa Kenya Marthe Karua akisema chama hicho na serikali haviwezi kuingilia masuala ya mahakama na kwamba wanaheshimu mgawanyo wa mamlaka.
Msingi wa kauli hiyo unatokana na jana Mwanasheria Matha, ambaye pia ni mwenyekiti wa chama cha siasa cha PLP, kutoa kauli kupitia mindandao ya kijamii akisema CCM na serikali wanaiogopa CHADEMA ndio maana wanamuweka ndani Tundu Lissu ili washinde kirahisi akiwataka kumuachia na kukaa meza ya mazungumzo.
Akijibu hoja hiyo leo mkoani Dodoma Wasira amesema Tanzania haivurugi amani ya Afrika Mashariki isipokuwa wanaendesha mambo yao kwa amani na salamu anazompatia ni kwamba aache kujipima na CCM, kwakuwa ni chama kikubwa Afrika.
"CCM haina hofu na chama chochote lakini hatuwezi kuingilia kazi ya Mahakama na hatuwezi kuingilia shughuli za Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi kwakuwa ni vyombo vyenye mamlaka. lakini kama ni mjuzi hivyo ashughulike na mambo ya Kenya," amesema Wasira.
Kulingana na Wasira aliyekuwa akizungumza hayo huku akishangilia na umma, amesema kama anaona chama chake ni kidogo na anataka umaarufu basi aangalie mataifa mengine ya Afrika yenye migogoro akatatue kama ilivyo Sudani ya Kusini.
"Akishindwa arudi nyumbani akaendeshe chama chake ambacho sera zake hazijulikani. Atuache Tanzania tuchaguane kwa utaratibu wetu hata mwenyewe na zungumza hapa nilichaguliwa kwa kishindo katika nafasi hii ndani ya chama naamini dozi hii inamtosha," amesema Wasira.
Amesema katika uchaguzi uliopita Kenya, Martha alikuwa mgombea Mwenza wa Raila Odinga walikuwa wanalalamikia uamuzi wa tume yao ya uchaguzi walienda hadi Supreme Cort lakini hawakupata kitu akaenda Mahakama ya Afrika Mashariki na alitoka.
"Kama alitoka amuache Lissu na kesi yake matokeo yatapatikana na yeye atayakubali kama alivyokuyakubali yale ya Kenya," amesema Wasira.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED