Wateja 14 wa Shirika la Umeme nchini TANESCO Mkoa wa Morogoro wamesitishiwa huduma ya umeme baada ya kubainika wakitumia miundombinu ya shirika hilo kinyume cha sheria.
Mhandisi Mkuu wa TANESCO, ukanda wa Morogoro Kaskazini,Mhandisi Adam Abdula, amesema zoezi hilo litaendelea kuhakikisha mali za umma zinalindwa.
Miongoni mwa waliokamatwa ni Salim Ally,mkazi wa Kijiji cha Madudu wilayani Kilosa mfanyabiashara wa mashine za kusaga, aliyedaiwa kutumia umeme kwa kujiunganishia nyaya bila kufuata utaratibu rasmi wa TANESCO.
Wananchi wakiwemo viongozi wa vijiji na mitaa katika wilaya za Kilosa, Morogoro Manispaa na Mvomero wamepongeza hatua hiyo ya Serikali kupitia TANESCO wakisema itasaidia kudhibiti wizi wa umeme na kulinda miundombinu ya shirika hilo.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED