Waziri wa Katiba na Sheria, Dk.Damas Ndumbaro amesema kutokana na mfumo wa haki kuimarishwa, kwa sasa msongamano wa mahabusu magerezani umepungua na kesi zinaendeshwa kwa kasi.
Dk.Ndumbaro ameyasema hayo leo jijini Dodoma katika uzinduzi wa jengo la Makao Makuu ya Mahakama, Tume ya Utumishi wa Mahakama na Nyumba za makazi ya Majaji.
"Mheshimiwa Rais umeimarisha sana sekta ya haki sio tu kwa kuunda tume ya haki jinai, lakini umetekeleza kwa vitendo na tunaona sasa msongamano magerezani umepungua na kesi zinakwenda kwa kasi" Dk.Damas Ndumbaro
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED