Rais wa Zanzibar, Dk. Hussein Ali Mwinyi (kushoto) na Rais wa Yanga ambaye pia ni Mwenyekiti wa Vilabu vya Soka Barani Afrika, Mhandisi Hersi Said Ali, wakiwa wameshika kombe
Rais wa Zanzibar, Dk. Hussein Ali Mwinyi, ameizawadia Klabu ya Yanga SC shilingi mil 100, kwa kutambua ushindi na mafanikio makubwa waliopata katika msimu wa mwaka 2024/2025.
Rais Mwinyi ameyasema hayo leo, Juni 30, 2025, alipokutana na viongozi pamoja na wachezaji wa Yanga waliofika Ikulu, kwa ajili ya kumkabidhi makombe matano ya michuano mbalimbali waliyoyatwaa msimu huu.
Akizungumza katika hafla hiyo, Rais Mwinyi amepongeza mafanikio hayo makubwa yaliyopatikana na klabu hiyo kongwe, akieleza kuwa yanajenga heshima na historia muhimu katika tasnia ya michezo nchini.Rais wa Zanzibar, Dk. Hussein Ali Mwinyi (kushoto) na Rais wa Yanga ambaye pia ni Mwenyekiti wa Vilabu vya Soka Barani Afrika, Mhandisi Hersi Said AliAidha, ameishukuru Yanga kwa kuendelea kuitangaza Zanzibar ndani na nje ya nchi kupitia kampeni ya Visit Zanzibar, huku akieleza kuwa hatua ya klabu hiyo kucheza baadhi ya michezo yake Zanzibar kunachangia kukuza uchumi na sekta ya utalii kutokana na kuongezeka kwa idadi ya wageni na wananchi kunufaika na fursa mbalimbali.