KAIKA kipindi kuanzia Julai 2024 hadi Februari 2025, serikali imesajili mashirika 939.
Mashirika hayo yametelekeza jumla ya miradi 405 iliyochangia upatikanaji wa huduma za kijamii ikiwemo afya, elimu, utunzaji wa mazingira, haki za binadamu na utawala bora kwa gharama ya shilingi bilioni 342.07.
Aidha, kulingana na tathmini ya mchango wa mashirika yasiyo ya kiserikali kwa mwaka 2023, jumla ya shilingi trilioni 2.6 zilitumika katika miradi mbalimbali ya maendeleo.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, amesema hayo leo, Aprili 9, 2025, bungeni jijini Dodoma, wakati akisoma hotuba ya Bajeti ya ofisi yake kwa mwaka wa fedha 2025/2026.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED