Meneja Mkuu wa Shirika la Masoko Kariakoo CPA Ashiraph Yusufu Abdulkarim amewataka watumishi wa shirika hilo kuhakikisha wanafanya mageuzi katika utendaji kazi kwa kuzingatia Sheria, Kanuni, Taratibu, Miongozo pamoja na taaluma zao ili kuleta matokeo chanya katika Shirika hilo.
Ametoa wito huo jana Jijini Dar es Salaam katika hafla fupi ya kukabidhiwa Ofisi na aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu Mary Maridadi.
CPA Abdulkarim amesema kuwa kila mtumishi anawajibika kusimama katika nafasi yake na kufanya kazi kwa bidi ili kufikia malengo ya Shirika hilo.
“Mtazamo wangu ni kwamba endapo watumishi watafanya kazi kila mmoja katika sehemu lake ni dhahiri kwamba uzalishaji utaongezeka na mazingira ya kazi yataboreshwa na kuleta ufanisi mzuri katika utendaji kazi wetu” ameeleza CPA Abdulkarim.
Vile vile CPA Abdulkarim amesisitiza nidhamu na uadilifu mahali pa kazi kuwa ni suala muhimu sana ambapo vikikaa sawa uleta matokeo chanya, kwani watumishi wanapokosa nidhamu na uadilifu wanaharibu taswira ya Shirika na hawawezi kutumia muda wao vizuri katika kutekeleza majukumu kikamilifu.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED