MWENGE wa Uhuru umezindua mradi wa maji wenye sh. bilioni 1.494 ambao unakwenda kuhudumia wananchi 6,407 wa vijiji vya Kwala na Mwembe Ngozi, Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha.
Meneja wa Wakala wa Maji na Usafi na Mazingira Vijijini (RUWASA) Wilaya ya Kibaha, Mhandisi Debora Kanyika, amesema mradi huo uliibuliwa na wananchi, baada ya changamoto ya kukosa huduma ya maji safi na salama, kutokana na uchakavu wa miundombinu iliyolengwa mwaka 1974.
Mhandisi Kanyika, amesema kabla ya mradi huo wananchi walikuwa wakitumia maji yasiyokuwa safi na salama ambayo yalikuwa yakiletwa na magari kwa gharama ya Sh. 300 kwa ndoo ya lita 20.
Meneja huyo amesema chanzo cha maji cha mradi huo ambao uko Kijiji cha Minazi Mikinda ni kisima chenye uwezo wa kutoa lita 43,000 kwa saa ambacho kina urefu wa mita 33.
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa, Ismail Ussi, akizindua mradi huo aliwataka wananchi kulinda miundombinu hiyo ya maji, ili iweze kutoa huduma kwa muda mrefu.
Salma Mohamed na Zainab Hussein ni kati ya wakazi wa Minazi Mikinda ambao wameishukuru serikali kwa utekelezaji wa mradi huo ambao umewapunguzia adha ya kutafuta maji mbali na makazi yao.
Salma amesema kwasasa wanaweza kufanya shughuli nyingine za maendeleo
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED