Wadau utalii wahimizwa uwekezaji sekta hiyo

By Christina Haule , Nipashe
Published at 04:40 PM Aug 05 2025
Uwekezaji wa magari ya utalii hukiuza mapato
Picha: Mtandao
Uwekezaji wa magari ya utalii hukiuza mapato

WADAU wa uhifadhi nchini, wamehimizwa kuwekeza kwenye mahoteli na usafaridshaji, ili kuimarisha suala la utalii nchini.

Mhifadhi kutoka Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Ruta Kihama, amesema hayo leo kwenye maonesho  ya wakulima Nanenane Kanda ya Mashariki, yanayofanyika mkoani Morogoro.

Amesema kuwa uwekezaji wa nyumba za kulala watalii jirani na hifadhi, utasaidia kuongeza nguvu za serikali katika kuendeleza uhifadhi na kukuza utalii.

Anasema pia uwapo wa magari ya kutosha utasaidia watalii wanaoendelea kuongezeka hifadhini kwa sasa, baada ya filamu ya Royal Tour iliyotolewa na Rais Samia Suluhu Hassan, kupata huduma kamili kwa wakati mzuri tofauti na ilivyo sasa.