Baadhi ya wajumbe wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutoka Kijiji cha Sokoni, Kata ya Sirari, wamelalamikia kuondolewa kwa majina yao kwenye orodha ya wapiga kura katika zoezi la kura za maoni, wakidai kuwa majina yao yamekatwa na kubadilishwa na ya watu wengine.
Wajumbe hao walionekana wakiwa nje ya lango la kuingia katika ukumbi wa Kanisa Katoliki ambapo kura hizo zilikuwa zinatarajiwa kupigwa, wakijieleza kwa Katibu wa CCM Wilaya ya Tarime, Hamza Keybanji.
Baada ya kusikiliza malalamiko yao, Katibu huyo aliagiza kuwa kila balozi wa nyumba kumi asimame na wajumbe wake halali ndipo waruhusiwe kupiga kura, kama njia ya kuhakikisha haki na uwazi katika mchakato huo.
Tukio hilo linaendelea kuonyesha changamoto zinazojitokeza katika zoezi la kura za maoni ndani ya CCM katika maeneo mbalimbali nchini, hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba 2025.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED