Mkurugenzi INEC ataka vyombo vya habari kutopendelea chama cha siasa

By Halfani Chusi , Nipashe
Published at 11:08 AM Aug 04 2025
Mkurugenzi wa Uchaguzi Tume Huru ya Uchaguzi (INEC) Ramadhani Kailima.
Picha:Mpigapicha Wetu
Mkurugenzi wa Uchaguzi Tume Huru ya Uchaguzi (INEC) Ramadhani Kailima.

Mkurugenzi wa Uchaguzi Tume Huru ya Uchaguzi (INEC) Ramadhani Kailima amevitaka vyombo vya habari kuripoti habari za uchaguzi bila kupendelea chama chochote cha siasa.

Kailima ameyasema hayo leo Agost 4 2025 wakati akifungua mafunzo kwa wanahabari wa vyombo vya Habari kuhusu uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika oktoba mwaka huu.

Kailima amesisitiza waandishi wa habari wasipotumia Kalamu zao vizuri wanaweza kuiingizia nchi katika machafuko.

Aidha,amewataka kuandika habari za kulinda amani ya nchi,kwa kutopandikiza chuki kwa kutumia vyombo vya habari.