PDPC: Tunashirikiana na jumuiya za kimataifa kulinda anga mtandao

By Enock Charles , Nipashe
Published at 12:08 PM Aug 04 2025
Mkurugenzi wa Usajili na Uzingatiaji wa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC), Stephen Wangwe.
Picha;Mpigapicha Wetu
Mkurugenzi wa Usajili na Uzingatiaji wa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC), Stephen Wangwe.

Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC ) imesema inashirikiana na jumuiya mbalimbali za kimataifa ili kulinda anga mtandao na madhara kwa wananchi.

Akizungumza wakati wa mafunzo kwa waandishi na wahariri wa vyombo vya habari Jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi wa Usajili na Uzingatiaji wa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC), Stephen Wangwe amesema kutokana na kila nchi kuwa na utaratibu wake katika masuala ya mtandaoni wameamua kubuni ushirikiano.

"Kuna kitu kinaitwa anga  ya kimtandao ambayo haina mipaka ya kijiografia na kulikuwa na changamoto ya usimamizi wake kumekuwa na uhitaji wa kuwa na Sheria zinazofanana katika nchi zote"

"SADC wametengeneza Sheria za mfano zinazotakiwa kutumiwa na nchi wanachama ili kuwe na usimamizi unaofanana katika masuala ya mtandao kwa lengo la kulinda anga ya mtandao" amesema Wangwe.