Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Doedatus Balile ameiomba serikali kuvitazama vyombo vya habari kwa jicho la huruma kwa kuwa hali ya uchumi ni ngumu sana.
Akizungumza leo Aprili 4,2025 wakati wa Mkutano Mkuu Maalum wa TEF unaoendelea sasa Mjini Songea, Balile alisema mkutano huo unafanyika chini ya kauli mbiu ya Uchaguz Huru na Haki.
“Uchumi wa vyombo vya habari ni mgumu mno, tunaomba serikali itupie jicho la huruma kwa kuwa vyombo vya ha ari ni muhimu sana kwa maendeleo ya nchi,”amesema.
Aidha, amesema TEF inaendelea kusisitiza matumizi sahihi ya majukwa ya kidijitali ili yatumike vizuri kwa maendeleo ya nchi.
“Aidha, amesema Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuhakikisha uhuru wa vyombo vya habari umeimarika tofauti na kipindi kilichopita jambo linalowezesha vyombo vya habari kufanyakazi kwa ukamilifu.
Aidha, amesema Dk.Emmanuel Nchimbi amekuwa mwenye utu kutokana na kuipenda tasnia ya habari tangu akiwa Waziri wa Habari, Sanaa na Utamduni, na kumuomba kutoiondoa roho yake ya utu aliyonayo.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED