Inaelezwa kuwa asilimia 61 ya Wanawake wote nchini wameolewa au wanaishi pamoja na wenza kama vile wameolewa, sawa na theluthi mbili huku Wanaume ikiwa ni asilimia 51 pekee.
Hii ni kwa mujibu wa Utafiti wa Demografia na Afya Tanzania wa Mwaka 2022 na Viashiria vya Malaria (TDHS-MIS) 2022 uliotekelezwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) na Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali (OCGS).
Utafiti huo unaeleza kuwa theluthi mbili ya wanawake sawa na asilimia 27 ya Wanawake wote Tanzania bado hawajaolewa huku wanaume ambao hawajaoa nchini wakiwa ni asilimia 44.
Kadhalika utafiti huo unataja asilimia 13 ya wanawake kuwa wameachwa, wametengwa, kuachika na wengine ni wajane.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED