"ENZI ya dhahabu ya Marekani inaanza hivi sasa...kuanzia leo, nchi yetu itastawi na kuheshimiwa...nitaiweka Marekani mbele." ni kauli aliyoitoa Rais wa Marekani Donald Trump muda mfupi mara baada ya kuapishwa huko Capitol Hill mjini Washington.
Kauli hii iliyotolewa Januari 20, 2025 ilianza kuoneka kupitia msimamo wake wa kupinga sera mbalimbali zilizokuwa zikisimamiwa na serikali ya nchi hiyo kupitia mtangulizi wake Joe Biden.
Hata hivyo, tangu Rais Trump achukue mamlaka rasmi Dola ya Marekani imezidi kupanda kila uchwao, kutoka Dola moja ikiuzwa kwa Sh. 2,474.2 Januari 20,mwaka huu hadi sasa ikielekea 2,700.
Kwa mujibu wa viwango vya kubadilishia fedha za kigeni iliyotolewa na Benki Kuu ya Tanzania (BoT), inauzwa kwa Sh. ilionesha kuwa Dola moja inauzwa kwa Sh.2474.2 Januari 20, 2025 hadi kufikia Sh.2622.5 Machi 9, 2025 kwa mujibu wa taarifa ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) huku mtaani ikiuzwa Sh.2700.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED