Makonda ataka ushirikiano Serikali na TLS

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 02:25 PM Mar 08 2025
MKUU wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda
PICHA: MTANDAO
MKUU wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda

MKUU wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda, ametaka kuwepo kwa ushirikiano kati ya Serikali na Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) ili kuimarisha msaada wa kisheria kwa wakazi wa mkoa huo.

Akizungumza jijini Arusha leo wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani , huku Rais Samia Suluhu Hassan akiwa mgeni rasmi, Makonda alielezea uwezo wa wanasheria takriban 882 katika TLS kwa mkoa huo kutoa msaada wa kisheria unaohitajika kwa jamii. 

“Wananchi wetu wengi hawana uwezo wa kumudu huduma za kisheria na mara nyingi hukumbana na dhuluma kwa kukosa uelewa wa kisheria, kwa kibali chako tunapanga kuwahamasisha mawakili hawa kutoa msaada, hadi kufikia Septemba mwaka huu tunalenga kuondoa migogoro ya kisheria inayotokana na kutojua sheria,” alisema.

Ushirikiano huu, alisisitiza, utawawezesha wakazi wa Arusha, kujenga jamii yenye taarifa zaidi kupitia juhudi za pamoja za serikali na TLS.