Lissu: Mfumo wetu wa uchaguzi unawafelisha wanawake

By Enock Charles , Nipashe
Published at 05:32 PM Mar 08 2025
MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu
PICHA: MTANDAO
MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu

MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu amesema mfumo uliopo wa uchaguzi nchini unafifisha juhudi za kuleta usawa wa kijinsia.

Akizungumza na wanawake wa chama hicho katika kilele cha maadhimisho ya  Siku ya Wanawake Duniani amesema kwa mfumo uliopo ni ngumu kwa wanawake kushindana na wanaume katika majimbo kwa kura za wananchi na badala yake kubaki kutegemea viti maalum. 

“Mfumo wetu wa kikatiba umewafelisha wanawake na ndio maana bila viti maalum uwepo wao bungeni ni chini ya asilimia 10” amesema Lissu  

“Katiba yetu inasema kutakuwa na usawa wa binadamu, Katiba yetu inasema watu wote ni sawa mbele ya sheria na inasema ni marufuku kubagua binadamu kwa misingi ya kijinsia”

 “Lakini ukienda kwa wananchi wanawake wanaopigiwa kura ni asilimia 9, pamoja na kwamba wapigakura wenyewe, asilimia zaidi ya 50 ni wanawake”

“Kwahiyo tunaposema no reforms no election sababu nyingine ni hii mfumo wetu wa uchaguzi hauwafai wanawake”