Rose Mayemba ataka wanawake kupewa fursa kwa kuzingatia weledi

By Enock Charles , Nipashe
Published at 03:48 PM Mar 08 2025
MJUMBE wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Rose Mayemba
PICHA: MTANDAO
MJUMBE wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Rose Mayemba

MJUMBE wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Rose Mayemba ametaka kufanyika marekebisho katika mifumo ya uchaguzi ili watakaopata nafasi za uongozi ikiwemo wanawake wapate kwa kuzingatiwa ujuzi wao.

Akizungumza katika kongamano la Baraza la Wanawake wa chama hicho, (BAWACHA) Rose amesema ili kuhakikisha usawa wa kijinsia inabidi kuwekwa mifumo sawa ikiwemo mifumo ya uchaguzi ili kuwa na uchaguzi huru na haki.

“Tunataka mifumo ya uchaguzi ibadilishwe ili kila atakayepata fursa asiipate kwa ajili ya jinsia yake bali aipate kwa sababu ya weledi alionao” amesema Rose.

“Kila mmoja ana wajibu wa kuilinda na kuipigania nchi yetu ili kupata mabadiliko ya kweli na uhuru wa kweli na kila mmoja kufaidi matunda mema ya taifa hili” amesema.