Rais Samia: Tutanunua umeme kwa ajili ya mikoa Kaskazini

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 03:01 PM Mar 09 2025
Rais Samia Suluhu Hassan
Picha: Mtandao
Rais Samia Suluhu Hassan

RAIS Samia Suluhu Hassan amesema kuwa serikali itanunua umeme, kwa ajili ya mikoa ya Kaskazini inayokabiliwa na kukatikakatika kwa nishati hiyo.

Akihutubia mamia ya wananchi Machi 9,2025 wakati wa uzinduzi wa mradi wa maji wa Mwanga, Same na Korogwe utakaohudumia vijiji 38 vyenye watu 300,000 uliogharimu zaidi ya Sh. bilioni 406.

“Natambua ukanda wa Kaskazini umeme ukanatikakatika, serikali iko kwenye hatua za mwisho kusaini mkataba wa kununua umeme uungwe ili wananchi wapate uhakika,” amesema.