RAIS Samia Suluhu Hassan amesema yeye si muumini wa kukata tama ndio maana amehakikisha mradi uliokwama kwa miaka 19 unakamilika na sasa utahudumia wananchi zaidi ya 300,000 wa vijiji 38 vya Mwanga, Same na Korogwe.
Kiongozi huyo ameyasema hayo Machi 9,2025 wakati akizindua mradi huo uliogharimu zaidi ya Sh. bilioni 406.06 ambazo ni mkopo wenye masharti nafuu kutoka Saud Arabia Fund na Kuwait Fund.
Mradi huo ambao ulianza upembuzi yakinifu mwaka 2006, kisha mkataba wa ujenzi ulisaniwa mwaka 2014 na baada ya kusuasua kwa muda mrefu mwaka 2024 umekamilika.
“Ila kwasababu huwa siamini kwenye kushindwa nilimwambia Waziri wa Fedha na Waziri wa Maji kuwa huu mradi lazima tuukamilike, tulikopa mkopo nafuu kuhakikisha wananchi wetu wanapata huduma hii muhimu.”
“Hakika haya ni mafanikio makubwa ambayo yanagusa kila nyanja za maisha yanaenda kupunguza umaskini, muda wa kutafuta maji, ili wananchi wafanyekazi zao nyingine za maendeleo na kuongezeka kwa muda wa wanafunzi hasa wa kike ambao wanatolewa mapema kwenda kutafuta maji,
Pia wanawake wa eneo hili ambao walikuwa wanakwenda kusaka maji kwasababu wengine yanapatikana ndani na wengine karibu ya nyumba zao, kuimarisha afya na kuepusha magonjwa yatokanayo na matumizi ya maji yasiyo salama, na utaimarisha uwekezaji kwa kuwa wapo ambao wanategemea sana maji.
“Nikiwa ofisini (kuingia madarakani) nilikuwa napata ugeni wa mara kwa mara wa Mzee Clioper Msuya, nilijua anakuja kunieleza kuhusu ABC za urais wakati huo, alinieleza shida zake ni mradi huu na barabara ya Baypass. Nilipita mara ya pili kumsalimia akaniambia, na mara ya tatu alikuja Chamwino Dodoma na akanieleza tena kuhusu huu mradi, nilimuahidi Juni mwaka jana ungekamilika, nashukuru maji ya awali yalinza kutoka.
OOOOO
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED