Dk Slaa aibukia BAWACHA awataka kudai mabadiliko mifumo ya uchaguzi

By Enock Charles , Nipashe
Published at 03:22 PM Mar 08 2025
Aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Sweden na Katibu Mkuu wa zamani wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk.Wilbroad Slaa
PICHA: MTANDAO
Aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Sweden na Katibu Mkuu wa zamani wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk.Wilbroad Slaa

ALIYEKUWA Balozi wa Tanzania nchini Sweden na Katibu Mkuu wa zamani wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk.Wilbroad Slaa hatimaye ameibukia katika kongamano la chama hicho na kuwataka kuendelea kudai mabadiliko katika mifumo ya uchaguzi.

Akizungumza katika kongamano la Baraza la Wanawake wa chama hicho BAWACHA, Dk.Slaa amesema hakuna haja kwa chama hicho kukubali mazungumzo yasiyo na uhakika bali kudai haki ya kupata mabadiliko katika mifumo ya uchaguzi.

“BAWACHA mjue kwamba hatuna muda wa kutosha na mabaraza mengine inabidi kurejea kwa watu wao kuwaambia watu wao kwamba no reforms no election” amesema Dk Slaa.