Joto kali na nyoka, Ilivyo hatari kwa makazi

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 02:23 PM Mar 09 2025
Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori Mweka, Bwana Tito Lanoy, akimdhibiti nyoka aina ya Koboko wa Kijani (Green Mamba) na kisha kumpeleka mbali na makazi ya watu ili asilete madhara
Picha: Mtandao
Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori Mweka, Bwana Tito Lanoy, akimdhibiti nyoka aina ya Koboko wa Kijani (Green Mamba) na kisha kumpeleka mbali na makazi ya watu ili asilete madhara

MKOANI Dar es Salaam, viwango vya juu vya joto kwa wiki moja mfululizo vililkuwa juu, kwa mujibu wa Mamlaka ya Hali ya ewa Tanzania (TMA).

Mkoa wa Dar es Salaam, viwango vya juu vya joto kwa wiki moja mfululizo, vilifikia nyuzi joto 35°C huku baadhi ya mikoa ambayo huwa na viwango vya chini zaidi kwa joto kama vile Mbeya na Arusha kukiwa na kati ya nyuzi joto 25°C na 26°C.

Mkufunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori, Mweka, Bwana Tito Lanoy, akimdhibiti nyoka aina ya Koboko wa Kijani (Green Mamba) na kisha kumpeleka mbali na makazi ya watu ili asilete madhara. Green Mamba ni nyoka mpole anayependa kukaa juu ya miti. Anakula ndege wadogo. Green Mamba ni nyoka mwenye sumu kali aina ya neurotoxic. Akimuuma mtu, sumu yake inashambulia mfumo wa fahamu hivyo kusababisha kifo kwa kushindwa kupumua
Hayo yakijiri, ushauri watolewa wa wataalamu wa wanayamapori kujikinga na wadudu wakali wakiwamo nyoka.

“Usilale au kukaa chini katika maeneo ambayo kunaweza kuwa na nyoka. Vaa buti za ngozi za juu wakati wa kutembea au kufanya kazi katika maeneo yenye mimea mnene.

“Usijaribu kukamata, kushika au kushika nyoka wenye sumu kali, ikiwa wewe si mtaalamu wa kushughulikia nyoka.

Kwa habari zaidi soma gazeti Nipashe Machi 10, 2025, fuatilia mitandao ya kijamii nipashedigital