Aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum katika Bunge la 12, Ester Mtiko, amemkumbuka Hayati Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Yustino Ndugai, kama mtu mwenye msimamo thabiti aliyelisimamia jambo bila kujali maoni ya wengine.
Mtiko amesema Ndugai alikuwa kiongozi aliyesimamia kanuni, sheria na taratibu katika uendeshaji wa Bunge, huku akiwa mlezi na baba kwa wabunge wake.
“Alikuwa ni kaka kwangu, baba na mliezi. Pale ambapo wabunge walipata fursa za kwenda kujifunza masuala mbalimbali, alikuwa anahakikisha wanashiriki na kunufaika na maarifa hayo ili yaweze kuishauri Tanzania,” amesema.
Mtiko pia ameeleza kwamba licha ya Ndugai kuwanyanyasa wabunge wa upinzani wakati fulani, alisimamia kwa uadilifu misingi ya uendeshaji wa Bunge bila upande wowote wa kisiasa.
“Nilikuwa mbunge wa upinzani, na tuliona kama anatunyanyasa, lakini sasa ukiangalia kwa kina, ulikuwa anatenda haki kwa misingi ya sheria na kanuni za Bunge,” amesema Mtiko.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED