Sigrada atangaza kuwania Jimbo Njombe Mjini

By Elizabeth John , Nipashe
Published at 05:19 PM Aug 11 2025
Sigrada Mligo
Picha: Elizabeth John
Sigrada Mligo

MWANACHAMA wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), Sigrada Mligo, ametangaza rasmi nia ya kugombea ubunge wa Jimbo la Njombe Mjini, kupitia chama hicho.

Washiriki mkutano huo
Sigrada, ametoa tamko hilo leo, Agosti 11, 2025, alipokutana na wanachama wa CHAUMMA mjini Njombe, pamoja na kikao hicho, chama hicho pia kiligawa kadi kwa wanachama wapya waliojiunga zaidi ya 100.