MWANACHAMA wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Lumola Kahumbi, amehamia Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA).
Akizungumza na waadishi wa habari leo kwenye ofisi za chama hicho, Kahumbi amesema miongoni mwa sababu zilizochangia ahame na kuhamia chama kingine ni pamoja na CHADEMA kukataa kushiriki uchaguzi mkuu mwaka huu.
Kadhalika, ametangaza nia ya kugombea ubunge jimbo la Bukene
"Msimamo wa CHADEMA wa 'No Reform No Election, umesababisha niondoke, mnafahamu kwamba kwenye siasa ukipotea ndani ya mwaka mmoja tu unafutika kwenye ramani."
Amesema CHAUMMA na CHADEMA havipishani sana kwenye mlengo wake, ndio maana ameamua kujiunga nacho tofauti na ambavyo angeenda kwenye chama kingine.
"Kusema CHAUMMA ni chama cha mkakati wa CCM, hizo ni propaganda tu.CHADEMA iliwahi kuitwa ni ya Wachaga, lakini tulikuwapo hata sisi Wanyamwezi. Iliitwa ya Wakristo, lakini siyo kweli."
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED