Hamad Rashid: Nitahakikisha wananchi wanakula na kushiba

By Rahma Suleiman , Nipashe
Published at 03:12 PM Oct 15 2025
Mgombea urais wa Zanzibar kupitia chama cha ADC Hamad Rashid Muhammed
PICHA: RAHMA SULEIMAN
Mgombea urais wa Zanzibar kupitia chama cha ADC Hamad Rashid Muhammed

MGOMBEA urais wa Zanzibar kupitia chama cha ADC Hamad Rashid Muhammed amesema kuwa Zanzibar haina sababu ya kununua mchele aina ya mapembe kutoka nje ya nchi hivyo akiongoza serikali atapiga marufuku uingizaji wa mchele huo visiwani humo.

Amesema atahakikisha wananchi wa Zanzibar wanakula na kushiba bila ya kulalamika njaa kama ilivyo sasa na visiwa hivyo vitakuwa na uwezo wa kuzalisha chakula. Hamad ameyasema hayo leo visiwani humo wakati akizungumza mawakala wa chama hicho ambao watasimamia uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

Hamad amesema kuwa anauwezo mzuri wa masuala ya uzalishaji wa chakula hivyo atahakikisha kuwa kilimo ndio kipaombele chake cha kwanza ili Zanzibar kujitosheleza kwa chakula. Amesema kuwa atahakikisha kuwa kilo moja ya mchele haizidi kuuzwa shilingi 1500 na Zanzibar itakuwa na mchele mzuri wa kutosha.