Mahakama Kuu yatupilia mbali ombi la Dada wa Polepole

By Grace Gurisha , Nipashe
Published at 06:26 PM Oct 15 2025
Ndugu wa aliyekuwa Balozi wa Malawi na Cuba, Humphrey Polepole, wakizungumza na wakili Peter Kibatala (kushoto) katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, wakati wa usikilizwaji wa shauri hilo
Picha: Imani Nathaniel
Ndugu wa aliyekuwa Balozi wa Malawi na Cuba, Humphrey Polepole, wakizungumza na wakili Peter Kibatala (kushoto) katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, wakati wa usikilizwaji wa shauri hilo

MAHAKAMA Kuu ya Tanzania Masijala Ndogo ya Dar es Salaam imetupilia mbali maombi ya dada wa Humphrey Polepole, Christina Polepole ya kutaka kutoa ushahidi kwa njia ya mdomo katika shauri la ndugu yake, kutokana na madai kwamba aliwekwa chini ya ulinzi na maofisa wa polisi.

Pia, Christina aliiomba Mahakama hiyo atoe ushahidi kwa njia ya mdomo juu ya madai kuwa aliwekwa chini ya ulinzi na maofisa wa Polisi, Julai 17, 2025

Ombi hilo la Christina liliwasilishwa leo na Wakili Kibatala mbele ya Jaji Mfawidhi Salma Maghimbi. Amesema Mahakama inakataa ombi hilo na badala yake Mahakama inatoa amri ya kwamba kesi iendelee kusikilizwa.

"Kwa sababu maombi hayo hayawezi kusababisha kusimamishwa kwa shauri lililopo mahakamani hapo kwa kuwa limeletwa chini ya hati ya dharura," amesema Jaji Maghimbi