Part 2: Bernard Mwakajila: Mwalimu asiye na taaluma atengeneza 'A' 100 somo la hisabati sekondari

By Halfani Chusi , Nipashe
Published at 01:00 PM Sep 01 2025
Part 2: Bernard Mwakajila: Mwalimu asiye na taaluma atengeneza 'A' 100 Somo la Hisabati sekondari.

Sehemu ya kwanza ya makala hii ilieleza simulizi ya kipekee ya Bernard Mwakajila, kijana aliyehitimu kidato cha sita lakini alishindwa kujiunga na chuo cha ualimu kutokana na ukosefu wa ada. Leo hii, jina lake limekuwa gumzo katika shule ya sekondari Kimara, Ubungo – jijini Dar es Salaam, baada ya kufanikisha mafanikio makubwa katika somo la hisabati.