Bernard Mwakajila, muhitimu wa kidato cha sita aliyeshindwa kujiunga na chuo cha ualimu kutokana na ukosefu wa ada, ameibua mwanga mpya katika somo la hisabati kupitia shule ya Sekondari Kimara, Wilaya ya Ubungo jijini Dar es Salaam. Juhudi zake za kujitolea kufundisha zimetoa matokeo makubwa, ambapo wanafunzi wamepata ‘A’ 100 katika mtihani huo unaoogopewa na wengi.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED