NLD kuzingatia kundi wenye ulemavu kwenye kampeni

By Grace Mwakalinga , Nipashe
Published at 05:15 PM Sep 01 2025
Mgombea urais Chama cha National League for Democracy (NLD), Doyo Hassan Doyo
Picha: Grace Mwakalinga
Mgombea urais Chama cha National League for Democracy (NLD), Doyo Hassan Doyo

MGOMBEA urais Chama cha National League for Democracy (NLD), Doyo Hassan Doyo, amesema kampeni zake kutakuwa na mkalimani wa lugha za alama, maandishi ya nukta nundu na miundombinu mingine rafiki kwa ajili ya watu wenye mahitaji maalumu.

Doyo ametoa kauli hiyo akizungumza na Nipashe Digital kuhusu maandalizi ya uzinduzi wa kampeni za NLD zinazotarajiwa kufanyika Septemba 4, 2025, jijini Tanga.

Amesema lengo la kuweka mkalimani na miundombinu mingine kwa watu hao, ni kuhakikisha sera zake zinayafikia makundi yote na kufahamu nini chama kimedhamiria, endapo watanzania watakipa ridhaa ya kuongoza nchi kupitia sanduku la kura Oktoba 29, 2025.