Vyama 17 kati ya 18 vilivyosaini kanuni za maadili ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu tayari vimeshasimamisha wagombea wa nafasi ya urais wa Zanzibar na kwenda kuchukua fomu katika Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Maisara.
Vyama hivyo ni CCM, NLD, AAFP, CUF, TLP, NRA, NCCR-Mageuzi, ACT Wazalendo, CCK, SAU, ADA-TADEA, UMD, UDP, ADC, MAKINI na DP. Chama pekee kati ya 18 kilichosaini maadili lakini hakijasimamisha mgombea wa urais Zanzibar ni Chama cha Mkombozi wa Umma (CHAUMA).
Kwa siku ya leo, Septemba 1, vyama vitano vilifika ZEC Maisara kuchukua fomu huku wagombea wake wakiambatana na wafuasi wao.
Kati ya wagombea hao 17, watatu ni wanawake na 14 ni wanaume. Hii ni tofauti na uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 ambapo hakukuwa na mgombea mwanamke kwa nafasi ya urais Zanzibar.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED